Habari

Zimbabwe yamuombea mke wa Rais Mugabe kinga ya kidiplomasia SA

Serikali ya Zimbabwe imemuombea mke wa Rais Mugabe kinga ya kidiplomasia dhidi ya kesi ya ushambuliaji inayomkabili nchini Afrika kusini.

Taarifa hizo zimetolewa na maofisa wa polisi wa taifa hilo leo asubuhi zikidai hayo yamefanyika kwa mujibu wa sheria.

“Grace Mugabe alikuwa bado yupo Afrika Kusini” iliongezea wakipinga ripoti za awali kwamba alikuwa amerudi nchini Zimbabwe.

Taarifa ya mtandao wa BBC Swahili,imesema kuwa,mwanamitindo mwenye umri wa miaka 20 amemtuhumu Grace Mugabe kwa kumshambulia katika hoteli moja mjini Johannesburg.

Polisi walitarajia kwamba mke huyo wa Mugabe angejisalimisha kwao mwenyewe siku ya Jumanne lakini hakufanya hivyo.

Hata hivyo Afrika Kusini bado ilikuwa inataka kuhakikisha kuwa kinga hiyo amepatiwa kulingana na sheria, ilisema taarifa hiyo.

Mazungumzo yalikuwa yanaendelea na mawawikili wa Mugabe na ubalozi wa Zimbabwe kuhusu swala hilo, ilisema taarifa.

Akizungumza mbele ya kamati ya bunge mapema, Kaimu Mkuu wa Polisi Lesetja Mothiba alisema kuwa Grace Mugabe anatakiwa aende mahakamni.

Hatahivyo,hajatoa tamko lolote tangu maaoisa wa polisi waanze kumchunguza kuhusu madai hayo ya unyanyasaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents