Habari

Zitto adai Spika Ndugai anataka kulizima sakata la Tundu Lissu

Mbunge machachari wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo Mh. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa Spika wa Bunge Job Ndugai ameibuka sakata lake yeye ili kutaka kufunika nguvu ya wananchi kuhoji juu ya kupigwa risasi Mbunge Tundu Lissu.

Spika Ndugai

Zitto Kabwe amesema hayo Jumatano hii mara tu baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai leo bungeni kusema anauwezo wa kumzuia Mbunge huyo asizungumze bungeni hadi mwisho wa bunge hilo kwani Zitto hawezi kupambana naye.

“Nimegundua Spika Ndugai ameibua mashtaka yangu ili kufunika ufuatiliaji wa wananchi kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi. Nimeamua sitawapa hilo” aliandika Zitto Kabwe kupitia mtandao wake wa Twitter
Spika wa Bunge Mhe.

Job Ndugai jana aliagiza Mbunge Zitto Kabwe pamoja na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea kufika kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kuhojiwa kutokana na kauli walizotoa hivi karibuni, jambo ambalo Zitto Kabwe anadai limeibuliwa kwa lengo la kupunguza nguvu ya wananchi kutohoji sakata la Tundu Lissu kupigwa risasi.

Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Dodoma siku chache zilipita ambapo mpaka sasa bado amelazwa hospitalini nchini Kenya kwaajili ya matibabu zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents