Burudani

Zitto ajipanga kuirejesha Kigoma Allstars kwenye chart

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amezungumzia changamoto alizokumbana nazo kupitia mradi wake wa Kigoma All Stars kwa mwaka 2014 kiasi cha kushindwa kutamba tena.

Kigoma-All-Stars-meeting

Akizungumza na 255 ya XXL ndani ya Clouds FM leo, Zitto amesema lengo la kundi hilo kwa mwaka 2014 lilikuwa ni kuwapa uwezo kupitia Saccos yao ambayo ingewapa fedha ambazo zitawasaidia wasanii wake katika kazi za muziki wao.

“Mambo yalikuwa ni mengi, actually mwaka 2013 tulifanya kazi kidogo lakini 2014 hatukufanya kazi kabisa na tulikuwa tunaplan vitu vikubwa na kwa mfano tulifungua Saccos,” amesema.

“Unajua moja ya challenge kubwa wasanii wanayo ni anafanya kazi nzuri anahitaji kurekodi, angalia kama Linex video yake ya Wema kwa Ubaya, ile mwenyewe asingeweza kwa sababu ya gharama ni kubwa. Kwahiyo nilikuwa nimeamua kwanza kuwaanzishia Saccos ambapo kulikuwa kuna fedha pale msanii akiwa na kazi yake, anatafuta tu mtu wa kutengeneza video na Saccos inalipa moja kwa moja. Mapato ambayo anayapata kutokana na ile kazi analipa kidogo kidogo kwenye ile kampuni ingewafanya wasiwe na wasiwasi kwamba nitafanya kazi yangu, nitaingia studio nitafanya video bila shida na ukaingiza kwenye soko,” ameongeza.

“Sasa hivi inabidi msanii afanye kwanza audio, audio iende then anakuja anafanya video akishakusanya kusanya hela kidogo, angalia kwenye Wema kwa Ubaya imetoka audio na video kwa pamoja kwa sababu kulikuwa na mtu ambaye aliweza kusupport. Siwezi kusupport wasanii wote kwa muda mmoja, kwa mfano kuna wasanii ambao nyimbo zao ningependa sana nionyEshe support, Alikiba wimbo wake wa Mwana, lakini nilishindwa kwa sababu video ya Alikiba haiwezi kulingana na wimbo wa Linex, ni video kubwa ya thamani kubwa. Kama unatumia milioni tano kwa Linex kwa Alikiba ni zaidi milioni kumi na tano. Kwahiyo Saccos ndo ingeweza kusolve matatizo kama hayo, ndio ilikuwa target yetu kwa mwaka 2014.

“Lakini 2014 ilikuwa na changamoto nyingi. Ni mwaka niliomuuguza mama na kumpoteza. Mwanzo wa mwaka zilikuwa ni vurugu kutoka kwenye chama changu cha Chadema, baadaye ndo tumeingia kwenye masuala ya Escrow. Kwahiyo nikawa nimebanwa muda wote. Kwahiyo hope mwaka huu nitaangalia namna ya kuwasaidia,” amesisitiza.

“Kuna watu wana idea nzuri wana nyimbo nzuri, Peter Msechu anahangaika na wimbo wake wa Nyota, ule ni wimbo unahitaji a lot of promotion lakini anahangaika mwenyewe. Najisikia vibaya sana kwa sababu huyu ni mtu ambaye ningeweza kumsupport na angeweza ku-move on yeye mwenyewe na kuna wengine ambao hawajatoa tena kazi. Abdul hajatoa tena kazi, Queen Dareen hajatoa tena kazi, Makomando hata kusikika sasa hivi hawasikiki, najua lakini wana kazi mpya lakini ni kazi ambazo tungeweza kuzi-support zingeweza kwenda mbali zaidi lakini ndo matarajio yangu ya kuweza kufanya mwaka huu kabla ya uchaguzi.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents