Habari

Zitto ataka Serikali kutangaza baa la njaa

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameitaka Serikali itangaze rasmi baa la njaa kwa mujibu wa sheria.

Zitto alitoa kauli hiyo Ijumaa hii katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Nkome mkoani Geita kupitia ACT-Wazalendo.

“Hali ya chakula nchini si nzuri. Wananchi mmeshuhudia namna bei za vyakula zinavyopanda kila siku. Bei ya sembe sasa kilo moja imefikia shilingi 1,600 pale Morogoro, kilo moja ya mchele ni shilingi 1,500, maana yake leo ugali na wali imekuwa bei inafanana. Gharama za maisha zitaendelea kupanda kutokana na uhaba wa chakula kuwa mkubwa”.

“Ninapendekeza serikali hatua muhimu ya kisheria ya kutangaza balaa la njaa nchini, tamko la balaa la njaa nchini litaisaidia serikali kupata bajeti ya dharula ya kununua chakula na kutoa uhuru kwa wakuu wa wilaya kutangaza maeneo yao kuwa yana njaa” .

Hivi karibuni Waziri wa kilimo, Charles Tizeba, walitofautiana na Zitto kuhusu hali ya chakula ambapo waziri huyo alisema hali ya chakula nchini ni shwari huku mbunge huyo wa Kigoma akisema ni mbaya.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents