Habari

Zitto awashauri Watanzania wasimamishe shughuli zao kwa dakika moja ifikapo saa 7 mchana

Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe amewashauri Watanzania kusimamisha shughuli zao kwa dakika moja ifikapo saa 7 mchana leo Septemba 7, 2018 ili kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu anayepatiwa matibabu nchini Ubelgiji.

Tundu Lissu akiwa na Zitto Kabwe (kulia)

Zitto ametoa ushauri huo kupitia ukurasa wake wa Twitter, ikiwa leo ni mwaka mmoja umepita tangu Lissu ashambuliwe kwa risasi jijini Dodoma Septemba 7, 2018 majira ya saa 7 mchana akitokea bungeni kwenda nyumbani kwake Area D.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents