Aisee DSTV!
SwahiliFix

Zitto Kabwe amjibu Bashe baada ya kukaribishwa CCM ‘Wajibu niliyojipa duniani ni kuiua CCM’

Mbunge wa Nzega Mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Hussein Bashe amemkaribisha ndani ya chama hicho mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe hii ni mara baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro kutangaza adhima yake ya kuachana na CUF.

Related image

Mbunge wa Nzega Mjini kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Hussein Bashe

 

Mara baada ya Zitto Kabwe kuponda hatua ya Mtatiro kujivua uanachama wa CUF na kutangaza nia ya kujiunga na CCM. kupitia ukurasa wake wa Twitter akiandika ”Mwingine naye amejitoa kwa sababu zile zile hewa.”

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe

Ndipo Bashe akatumia nafasi hiyo kumkaribisha Zitto kujiunga na chama hicho cha Mapinduzi CCM ”Kaka na ndugu yangu Zitto Kabwe karibu CCM, wakati mwingine ni rahisi kuleta mabadiliko ya haki, demokrasia na maendelei ukitokea ndani ya CCM kuliko kuyatafuta nje.”

Naye Mh Zitto akajibu kuwa ”Wajibu nimejipa duniani ni kuiua CCM ili kukata mnyororo wa  ‘underdevelopment” nchini kwetu. Nikishindwa mimi watafanya kizazi kijacho Lakini CCM itatoka tu. Hakuna marefu yasiyo na ncha.”

 

Related Articles

9 Comments

  1. Mmh labda ufe ww lakin kwa ccm tena jina sio mtu kama unavyosema ww manae ccm haijulikan mwenyewe ni nan watu wanaiyona ipo naitaendelea kuwepo mababu na mabibi wamewacha sembuse ww ndugu yangu angalia tu familia yako siasa haina kwao ndomana kuna watu wana uwezo ila hawawaz siasa kabisa kwanza yatia ugonjwa wa moyo kwa upeo rabda makufuli anastarehe kag zaid yakupewa maneno machafu ataman leo akivue hicho cheo hana jins tu kama vip unda kampen yakusaidia watoto yatima upate swawabu itakua her kuna watoto wanahaha tu mitaan hawajui pakushika

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW