Habari

Zitto Kabwe avunjwa moyo na Spika Ndugai, mwenyewe afunguka ‘namuomba Mungu ampe uhai’

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai amemkatisha tamaa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa kumwambia kuwa hawezi kuwa Rais wa Tanzania.

Image result for Zitto kabwe vs spika ndugai
Zitto Kabwe na Spika Ndugai

Spika Ndugai, ameitoa kauli hiyo juzi Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kujadili muswada wa vyama vya siasa nchini, ambapo alimkatiza Waziri wa zamani wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene ambaye alikua akichangia muswada.

“Mheshimiwa Simbachawene bahati nzuri Zitto hawezi kuwa Rais wa nchi haiwezekani.” alisikika Spika Ndugai akimkatiza Simbachawene.

Hata hivyo, Spika Ndugai alifafanua kauli yake au kutaja sababu hasa itakayopelekea kiongozi huyo na chama chake kushindwa kushika dola.

Mhe. Simbachawene wakati akichangia muswada huo, alimtolea mfano kiongozi huyo wa ACT – wazalendo kuwa Rais wa nchi, huku akihoji atajisikiaje kama akishuhudia wapinzani wake wakiendesha shughuli za maandamano.

Kwa upande mwingine, Zitto Kabwe amemjibu Spika Ndugai kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kumuombea aishi maisha marefu ili aje ashuhudie utawala wake.

“Namwomba Sana Mungu ampe uhai Bwana Job Ndugai na pia anipe uhai na kama kuna kheri ndani yake anipe nafasi ya kusaidiana na wenzangu kuongoza nchi yetu. Hakuna ajuaye ya kesho isipokuwa Mungu tu,“ameandika Zitto .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents