Zitto Kabwe ayabana makampuni ya simu yataje mapato yanayopata kwa mauzo ya miito ya simu

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameendelea kuyabana makampuni ya simu nchini yataje mapato yanayoingiza kutokana na biashara ya miito ya simu, Ringback tone (RBT).

kabwe

Akitumia mtandao wa Twitter kuyabana makampuni hayo ambayo hata hivyo hayajamjibu mpaka sasa, mbunge huyo ameahidi kulishughulikia suala hilo hadi lifahamike wazi.

“Naomba majibu yenu waungwana. Mapato ghafi ya biashara ya #ringbacktones #RBT kwa mwaka,” alitweet kuomba majibu kutoka kwa makampuni hayo.

“Nawauliza tena #vodacom #airtel na #tigo je, mnaweza kuweka wazi mapato yenu kutoka biashara ya #RBT (#ringtones) #UWAZI,”aliongeza.

“Ninaponunua wimbo kama #RBT pia ni kumpa tafu msanii. Ninataka kujua kutoka kwenu mabwana.”
Baada ya kutopata majibu, Zitto alisisitiza, “Nitawasakama mpaka mseme, muweke wazi, mapato yenu ya RBT dhidi ya wasanii. Halafu Waziri @JMakamba atawashukia.”

Inadaiwa kuwa makampuni ya simu huingiza zaidi ya shilingi milioni 80 kila moja kwa siku kutokana na matumizi ya nyimbo za wasanii kwaajili ya ringtones na kwa mwaka makampuni hayo kwa pamoja huiingiza zaidi dola bilioni moja zinazotokana na huduma yanayozitoa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents