Habari

Zitto kwenda Mahakamani kupinga uteuzi wa Rais Magufuli

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) amesema Jumatano hii ataenda Mahakamani kupinga uteuzi wa nafasi ya Katibu wa Bunge uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli Jumamosi iliyopita.

Uteuzi huo ulienda sambamba na uteuzi wa Mawaziri ambapo baadhi ya mawaziri walibadilishwa na wengine kuongezwa.

“Katika kulinda utawala wa sheria nchini kwetu, pia Uhuru na Hadhi ya Mhimili wa Bunge, Leo tarehe 11/10/2017 tunawasilisha mahakamani ombi la kutengua uteuzi wa Katibu wa Bunge na kutaka mchakato wa kisheria ufuatwe katika kumpata Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” aliandika Zitto Facebook.

Rais Magufuli alimteua Katibu mpya wa Bunge na yule ambaye alikuwa akifanya shughuli hiyo kuahidi kumpangiwa kazi nyingine.

Zitto alisema uteuzi wa Katibu wa Bunge uliofanywa na Rais John Magufuli ni batili Kwa mujibu wa Sheria ya Utawala wa Bunge, sheria namba 14 ya mwaka 2008 ikisomwa pamoja na Katiba ya JMT ibara ya 87.

Alisema Katiba inatoa Mamlaka Kwa Rais kuteua na sheria inaweka utaratibu Wa kutekeleza mamlaka hayo ya Katiba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents