Michezo

Zlatan ahusishwa kukipiga klabu hii barani Afrika, afisa habari wa timu hiyo atoa neno

Klabu ya Pyramids FC inayoshiriki ligi kuu nchini Misri imehusishwa kutaka kumsajili mshambuliaji hatari wa LA Galaxy, Zlatan Ibrahimovic mwishoni mwa msimu wa ligi kuu Marekani  MLS.

Vyombo mbalimbali duniani vimeripoti habari hiyo ya Zlatan kutimkia Afrika ndani ya klabu ya Pyramids FC huku taarifa hizo zikiwashtua mashabiki wengi wa soka duniani.

Kwa mujibu wa tovuti ya RECORD  ambayo ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuripoti kuwa bilionea wa klabu hiyo, Turki al-Sheikh ambaye ni kipenzi cha mchezaji huyo analengo la kuwapatia washabiki zawadi ya Christmas na si kitu kingine bali ni kumsaini Zlatan Ibrahimovic.

Hata hivyo msemaji wa timu hiyo, Ahmed Hassan amekanusha vikali habari hizo akisema kuwa hawana mpango wa kumsajili Zlatan.

”Hatuna mpango wa kumsajili, Zlatan Ibrahimovic, yeye ni mchezaji mzuri lakini hakuna makubaliano yoyote kati yetu. Hatuna makubaliano na klabu ya Huddersfield Town juu ya winga wake Ramadan Sobhi au hata bekei wa WBA, Ahmed Hegazi,” amesema msemaji wa Pyramids FC, Ahmed Hassan akizitolea ufafanuzi tetesi zote zilizokuwa zinahusishwa ndani timu hiyo.

Zlatan ambaye amejiunga na LA Galaxy inayoshiriki ligi kuu Marekani akitokea Manchester United amefunga jumla magoli 16 katika michezo 21 aliyocheza huku mkataba wake ukimalizika mwaka 2020.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents