Michezo

Zlatan amchana Ronaldo baada ya kusema anafuata changamoto mpya Juventus “Changamoto ni kwenda timu ya daraja la kwanza na kuisaidia kuwa bingwa sio Juventus”

Baada ya Cristiano Ronaldo kuhama Real Madrid na kwenda timu ya Juventus ya nchini Italia, alipohojiwa alinukuliwa akisema kuwa ameamua kujiunga na timu hiyo ikiwa ni sehemu ya kubadilisha maisha na kutafuta changamoto mpya katika maisha ya kazi yake ya soka ambayo amekuwa akiifanya kwa muda mrefu. 


Ronaldo alifika mbali zaidi na kuamua kumshawishi kwa kutoa kauli hadharani mpinzani wake Lionel Messi nae kujaribu kuhama timu ili kutafuta changamoto mpya katika kazi yake ya soka, kwani Lionel Messi amekuwa akicheza timu moja tu FC Barcelona kwa miaka yote ukilinganisha na Ronaldo aliyewahi kucheza Ligi ya kwao Ureno, England, Hispania na sasa Italia. 


Sasa mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic ameikosoa kauli ya Ronaldo kuita Juventus ndio sehemu aliyokwenda kupata changamoto mpya huku ikidaiwa kuwa katoa kauli kuwa Messi hana haja ya kuhama Ligi ndio adhihirishe ubora wake, Ronaldo kama angetaka changamoto mpya basi angeenda timu ya madaraja ya chini na kuhakikisha inapanda Ligi Kuu na kutwaa Ubingwa. .


“Cristiano Ronaldo anazungumzia kuhusiana na changamoto mpya? Anaita ni changamoto mpya Kwenda klabu ambayo tayari ni kawaida kushinda Serie A? kwa nini asingeamua miaka michache iliyopita kwenda katika timu ya daraja la pili na kuisaidia kupanda Ligi Kuu na hatimaye kupanda na kutwaa Ubingwa? Kujaribu kuwa Bingwa na timu ya daraja la pili na kuipeleka juu hiyo ndio anaweza kuita changamoto” alisema Zlatan Ibrahimovic 


Kwa upande wa Ronaldo kwa sasa akiwa na Juventus ambayo ndio msimu wake wa kwanza ndio anaongoza katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu ya nchini Italia akiwa tayari amepasia nyavu mara 14 akifuatiwa na Krzysztof Piatek anayecheza timu ya Genoa akiwa amepasia nyavu mara 13.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents