Zlatan Ibrahimovic ni moto Marekani, ainusuru LA Galaxy kutoka kwenye kipigo hadi ushindi

Zlatan Ibrahimović ameanza kuwasha moto katika ligi ya Marekani akiwa na klabu yake mpya ya LA Galaxy.

Mchezaji huyo ambaye usiku wa kuamkia leo amecheza mchezo wake wa kwanza katika ligi hiyo dhidi ya Los Angeles.

Katika mchezo huo ambao Zlatan aliingia dakika ya 71 wakati Galaxy ikiwa nyuma ya mabao 3-1. Lakini mshambuliqji huyo huyo raia wa Sweden alifanikiwa kufunga mabao mawili na kufanya mpaka mwisho wa mchezo LA Galaxy kuibuka na ushindi wa mabao 4-3.

Baada ya kutamba na jina la ‘Lion’ wakati akiwa Manchester United, Zlatan kwa sasa ameamua kutujifananisha na Red Wine kutokana na kuwa hatari kwenye kufunga mabao kadri umri wake unavyozidi kusonga mbele.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW