Zucckerberg aanza mwaka kwa kuingiza mabilioni

Ikiwa zimepita siku 10 tu toka tuanze mwaka huu wa 2018. Mwanzilishi wa Facebook Mark Zucckerberg ameshaingiza kiasi cha dola bilioni 4 kulingana na orodha ya mabilionea ya Bloomberg.

Ripoti zinasema, ‘Fahirisi kubwa za soko ni juu ya 2% ya mwaka hadi sasa. Zuckerberg mwenye umri wa miaka 33 ameshaingiza kiasi cha dola bilioni 4.16 tangu mwaka 2018 ulipoanza, na hisa za kampuni zinaongezeka zaidi ya 5% . Zuckerberg sasa amehamia kutoka 5 hadi 4 kwenye orodha ya mabilionea ya Bloomberg na sasa ana thamani ya karibu dola bilioni 77.

Bloomberg Billionaires kila siku kinataja watu matajiri zaidi duniani. Takwimu zinasahishwa mwisho wa kila siku ya biashara huko mjini New York.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW