Bongo Movie

Zuku Swahili Movie yawapa ubalozi JB na Aunt Ezekiel



Mambo yanazidi kuwanyookea wasanii wa filamu nchini almaarufu Bongo Movies ambapo waigizaji Jacob Stephen aka JB na Aunt Ezekiel wameteuliwa kuwa mabalozi wa Zuku Swahili Channel.
Channel hiyo itakuwa ikirusha filamu zinazotumia lugha ya Kiswahili, na nyingi zikiwa zile zinazosambazwa na kampuni ya Steps ya jijini Dar es Salaam.
Steps Entertainment Limited ni ‘official dealers’ wa Zuku TV upande wa Tanzania.
Mkurugenzi wa Zuku Tanzania, Johnson amesema hiyo ni hatua kubwa kwa tasnia ya filamu nchini ambapo itazitangaza filamu hizo na kukuza lugha ya Kiswahili kwa kupitia channel hiyo.
Uzinduzi rasmi wa Zuku Swahili Movie utafanyika mwezi ujao, ambapo channel hiyo itakuwa ikionekana kupitia king’amuzi cha Zuku.
Ujio wa Zuku Swahili Movie umekuja mwaka mmoja baada ya DSTV kuanzisha channel ya Africa Magic Swahili. Hata hivyo wasanii wa filamu nchini wamekuwa wakilalamikia malipo kidogo yanayotolewa na DSTV kwa kuonesha filamu zao.
Pictures Courtesy of Filamu Central.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents