HabariUncategorized

‘ Zuma amewaambia ANC kwamba haendi popote’ Malema

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameendelea kusisitiza kwamba amekwisha zingatia maelekezo yote ya kisheria na hawezi kuachia madaraka hayo. kwa mujibu wa viongozi wa upinzani Julius Malema na Bantu Holomisa.

Kitu hichi kilitokea baada ya mkutano ambao ulifanyika kati ya Zuma na viongozi 6 waliochaguliwa kwenye chama cha ANC siku ya Jumapili.

“Alikataa kujiuzulu na amewaambia wafanye uamuzi wa kumtoa kama watapenda kufanya hivyo kwa sababu hakuwa na hakuna kitu chochote kibaya alicho kifanya kwenye nchi hiyo. Analalamika kuwa alikubali maelekezo yote ya kisheria ikiwa ni pamoja ya kulipa fedha, Je, wanataka nini zaidi kutoka kwake.” Malema wa EFF aliandika katika akaunti yake ya Twitter.

Watu wamependekeza kwamba Cyril Ramaphosa, aliyechaguliwa kuwa rais wa ANC mwezi Desemba 2017, kuchukua nafasi ya urais wa nchi kabla ya uchaguzi mkuu ujao mwaka 2019. maandamano dhidi ya Zuma yanatarajiwa katika kufanyika makao makuu ya ANC yaliyopo huko Johannesbur, South Africa.

kulingana na taarifa za hivi punde ni kwamba Kamati ya wanachama wa ANC wanatarajia kufanya mkutano maalum mchana huu.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents