Burudani

RECAP: Album ya Harmonize ni hasara kibiashara (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz kwa mara ya kwanza ameichambua Album ya Harmonize.

ameichambua album hiyo huku akijaribu kulinganisha na wasanii wenzatu wa Nje ya Tanzania hasa Nigeria wanavyojua kuwekeza kwenye biashara ya muziki.

anasema mpaka sasa Album ya Harmonize ina siku 7 tangu kutoka na kwa mara ya kwanza Harmonize ameachia nyimbo kwa siku 7 hajafikisha angalau Viewers laki moja kwa wimbo mmoja.

anasema kuwa ukija kibiashara Album ya Harmonize ni Hasara kwani hata yeye anaonekana kuikatia Tamaa maana hata Promo hafanyi.

Anaongeza kuwa Target ya Harmonize ni kufanya Show za Kampeni za Siasa lakini Kimuziki album hiyo haimpeleki popote.

Ndani ya siku 7 wimbo wenye Viewers wengi ni 76k hii ni aibu kwa msanii kama Harmonize kufeli kibiashara kwa kiasi hiki kikubwa.

Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents