Habari

Ndege ya Makamu wa Rais yatoweka

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amelazimika kufuta safari yake ya kuelekea Bahamas baada ya ndege iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Chilima na Watu wengine tisa kutoweka wakati Makamu huyo wa Rais akielekea kuiwakilisha Serikali katika mazishi ya Waziri wa zamani Ralph Kasambara.

Ndege hiyo ya Jeshi la Ulinzi la Malawi ilitoweka kwenye rada baada ya kuondoka katika Mji Mkuu wa Nchi hiyo, Lilongwe, mapema leo ambapo tayari Rais ameamuru operesheni ya utafutaji na uokoaji baada ya Maafisa wa anga kushindwa kuwasiliana na ndege hiyo ———> “Wananchi wataarifiwa kuhusu maelezo yoyote kuhusu hali hiyo ukweli unapothibitishwa, sababu ya kutoweka kwa ndege hiyo bado haijajulikana”

Chilima mwenye umri wa miaka 51, amekuwa Makamu wa Rais wa Malawi kwa miaka kumi tangu mwaka 2014 na ni Baba wa Watoto wawili

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents