Habari
Mtandao wa Wanawake laki moja waendelea kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi
Mtandao wa Wanawake laki moja waendelea kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi wamuunga mkono Rais Samia
Mlezi wa Mtandao wa Wanawake laki moja Tano Seif Mwera ameendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya gesi ameyasema hayo alipokuwa katika Soko la Temeke Sterio alipokuwa akiongea na akina Mama lishe.
Mama lishe wa eneo hilo wame washukuru wanawake laki moja juu ya elimu waliyowapa ya matumizi ya nishati safi ya gesi wameiomba Serikali katika kuwasaidia kuwapa Majiko ya Gesi ya kupikia kwani wanaamini wakipata nishati safi mambo yanaweza kuwa mazuri zaidi katika baishara zao.