Dj Char4prezzy wa South Kukiwasha Leaders Club
DJ mkali wa amapiano kutoka nchini Afrika Kusini DJ @char4prezzy Jumamosi hii ya Disemba 07, atakuwa kwenye list ya watakaokonga nyoyo za wote watakaojitokeza kwenye usiku wa kiburudani wa Bata la Disemba unalofanyika Viwanja vya Leaders, Dar Es Salaam.
Baada ya kushuka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Dj huyo amesema kuwa anafurahia kuja na kuperfom Tanzania kwani mara zote alizokuja amekuwa akipata ushirikiano sana.
Na nyakati hii ameeleza namna anavyomkubali msanii na dancer Chinno Kidd huku DJ Char4prezzy akitamani atakapopanda jukwaani akutane na Chinno pamoja na kundi lake.
Bata la Disemba limeanza Ijumaa ya Disemba 06, likitarajiwa kuisha Jumatatu Disemba 08, alfajiri. Ambapo likiratibiwa na kampuni ya Heineken na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam .