Burudani

50 Cent ampindua vibaya P Diddy

Rapa kutoka nchini Marekani anatarajia kurithi mikoba ya P Diddy baada ya kampuni ya vinywaji ya (Vodka Ciroc) kumfuta ubalozi P Diddy.

Kwa mujibu wa (Takeout Media) imeeleza kuwa kampuni hiyo iko kwenye mchakato wa kuisaka saini ya 50 Cent ili kuwa kiongozi wa chapa hiyo ambapo atalipwa dola 100 milioni ikiwa ni sawa na Tsh 257.5 Bilioni.

Endapo dili hilo litakamilika basi itakuwa ni kampuni ya pili ya Vinywaji kwa 50 Cent kuwa balozi, kwa sasa ni balozi wa Kampuni ya Vinywaji viitwavyo (Branso Cognac).

Ikumbukwe kuwa mwezi Januari mwaka huu Kampuni ya vinywaji hiyo ilithibitisha haitafanya kazi tena na P Diddy ikidai kuwa Msanii huyo wa Hip-hop alishindwa kutimiza majukumu yake ya kimkataba.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents