BurudaniFahamuLifestyle

Abeba tuzo ya Uongo zaidi Duniani

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni wakati baadhi ya watu wakikemea vikali tabia ya kusema uongo, Fahamu kuwa kila mwaka ifikapo Novemba katika mji wa Santon, Uingereza HUFANYIKA shindano la kumtafuta mtu muongo zaidi Duniani “The World Biggest Liar”.

Katika shindano hilo washiriki wanapima uwezo wao wa kusema uongo kwa njia ya ubunifu na kufurahisha. Licha ya kuwa shindano hufanyika Uingereza lakini washiriki hutoka sehemu mbalimbali dunia.

Shindano hilo limewekwa kwa lengo la kuburudisha na kukuza vipaji vya watu katika kusema hadithi za uongo na kuzisimulia mbele ya jopo la waamuzi.

Kanuni na sheria za shindano washiriki wanapaswa kuwasilisha hadithi zao za uongo kwa wakati, kila mmoja anapewa dakika chache kuhadithia uongo huo unaweza kuwa hadithi yoyote lakini inapaswa kuwa ya kujenga na kuhamasisha.

Washindi hupatiwa tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na medali na heshima katika jamii. Pia washindi wanapewa nafasi ya kuandika hadithi zao kuziwasilisha katika majukwaa ya burudani.

Kati ya waliowahi kushindaa shindano hilo ni Philip Gate, Mike Naylor, Glen Boylan, Johnny Liar na Abrie Krueger

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents