AfyaHabari

Abiria ajifungua mtoto ndani ya ndege

Katika hali isiyotarajiwa, mwanamke mmoja amejifungua mtoto katika ndege ya shirika la ndege la Uholanzi KLM iliyokuwa ikitokea Ecuador kuelekea Amsterdam.

Habari hiyo ni kwa mujubu wa abiria waliomsadia. Inaelezwa muda mfupi kabla ya ndege hiyo kutua Jumatano, abiria huyo alianza kuhisi uchungu na akaenda msalani.

Lakini baada ya muda mfupi akajifungua mtoto wa kiume.Katika ndege hiyo kulikuwa na madaktari wawili na muuguzi mmoja kutoka Austria ambao waliweza kumsaidia.

Kwa mujibu wa hospitali, mama huyo anaeendelea vizuri alimpa mtoto wake jina la mmoja wa watu waliojitokeza kumsaidia la Maximilian.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents