Michezo

Abuya, Aziz wapewa angalizo

Klabu ya Yanga imewapa angalizo wachezaji wake wapya ambao wameonekana kung’ara katika mechi dhidi ya Augsburg ya UJerumani  kuwa makini na sifa zinazotolewa na mashabiki na mitandao ya jamii kwani zinaweza kuwaharibu na kupoteza ubora wao.

Wachezaji waliosifiwa zaidi katika mchezo huo uliochezwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa MBombela na Yanga kulala kwa mabao 2-1 ni Duke Abuya Mkenya aliyesajiliwa kutoka Singida Black Stars na Aziz Andambwile ambaye ni mchezaji mpya kutokea Singida Fountain Gate.

Pamoja na kuangukia kichapo hicho wachezaji hao waliotokea benchi walionyesha viwango vya hali ya juu na kuibadilisha timu kipindi cha pili.

Akizungumza jana kutoka nchini Afrika Kusini ambako timu hiyo ipo kwa michezo kadhaa ya kirafiki ya kimataifa Meneja wa timu hiyo, Walter Harrison alisema baada ya mechi hiyo na baadhi ya wachezaji kuonyesha viwango vya juu wamekyuwa wakimwagiwa sifa kemkemu hasa kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

“Hatutaki sana wachezaji wetu wapya waingie kwenye mambo ya mitandao ya kijamii hasa kusifiwa kwa sababu yanaweza kuwatoa mchezoni, tunachotaka kuhakikisha wanaelekeza nguvu na akili zao kwenye lengo mama la kufanya vema mazoezi na kuileta timu manufaa.

“Haya yanayoendelea kwenye mitandao yanaweza kuwafanya wakabweteka na baadaye wasifanye vizuri kwetu sisi hayana umuhimu na hatuyaangalii tunataka atimize majukumu yake uwanjani hayo ya kutrend tunawaachia watu wa mitandaoni” alisema Walter Harrison.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents