Habari

Adanganya kutekwa apate pesa ya kulipa deni

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia kijana aitwae Dickson Mungulu kwa tuhuma za kujiteka na kujipa majeraha mwilini mwake  ili aishawishi familia yake  kumtumia shilingi milioni tatu ambayo aliandika ujumbe mfupi wa maneno yaani (SMS) ili ionekane Wwatu wanaomshikilia ndio wanaitaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema walipofanya mahojiano ya kina na  Mtuhumiwa alikiri kufanya udanganyifu huo  kwa lengo la kupata pesa  aweze kulipa madeni yanayomkabili.

“Polisi ilipokea taarifa kutoka kwa Mtu mmoja ambae jina lake tunalihifadhi akidai Ndugu yake aitwae Dickson mwenye umri wa miaka 26 ametekwa na wamezipata taarifa kupitia ujumbe mfupi wa maneno uliotumwa kutoka kwenye simu ya Dickson kwamba watume shilingi milioni 3 vinginevyo atauwawa”

“Baada ya kupokea taarifa hizo Polisi walifanya uchunguzi kwa kina na tarehe 28 July majira ya jioni tulifanikiwa kumpata Kijana aliyesadikika kwamba ametekwa eneo la Mworombo Arusha akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni ambayo jina tumelihifadhi”

“Dickson aliemaliza shahada ya elimu katika Chuo Kikuu cha Makumira Arusha mwaka 2020 ilibainika alidanganya kwa kujiteka ili apate hiyo pesa ikamsaidie kulipa madeni, Polisi wanaendelea na upelelezi na ukikamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali kwa ajili ya hatua za kisheria.

By-BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents