Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemtangaza Adel Amrouche kuwa kocha Mkuu wa Taifa Stars.
Amrouche ambaye ni raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria amewahi kuzinoa timu mbalimbali kama Harambee Stars (timu ya Taifa ya Kenya) ambayo aliipa ushindi wa Cecafa 2013. Equatorial Guinea, Botswana, Libya na Yemen.
Kwa upande wa klabu amezinoa USM Alger, RC Kouba na MC Algiers.