FahamuHabari

Adnan Syed aachiwa huru baada ya kukaa gerezani miaka 25 akisingiziwa kumuua mpenzi wake

Aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya upili Baltimore, Maryland nchini Marekani Adnan Syed Mnamo 1999, alipatikana na hatia ya kumnyonga na kumuua mpenzi wake wa kipindi hicho Hae Min Lee baada ya kuhukumiwa maisha jela.

Kesi hiyo – ambapo upande wa mashtaka ulimtaja Syed mpenzi mwenye jeuri na mwenye wivu ambaye alimuua kikatili mwanamke wake ilivuta hisia za watu wengi.

Siku ya Jumatatu, jaji wa Maryland alibatilisha hukumu yake na kuweka tarehe ya mwisho ya kusikilizwa kwa kesi mpya.

Hukumu ilifutiliwa mbali katika kesi ya mauaji ya Kwa takriban miaka 25 .

Zaidi ya muongo mmoja baada ya Syed kufungwa gerezani, Rabia Chaudry, wakili anayeishi Baltimore na rafiki wa familia wa Syeds, mwaka 2014 alituma barua pepe kwa mwandishi wa habari anayeitwa Sarah Koenig na kumtaka achunguze upya mauaji ya Lee.

 

Mfululizo huo ulisema kwamba Syed, ambaye ni Mwislamu, alihukumiwa, kwa sehemu, kwa sababu ya upendeleo wa rangi.

Hatimaye ilifichua kuwa uchunguzi wa kitaalamu haukupata alama yoyote ya DNA yake kwenye mwili wa Lee wakati wa mauaji hayo.

Familia ya Lee ilikataa kushiriki katika uchunguzi huo na daima imekuwa ikishikilia kwamba wanaamini Syed alihukumiwa kwa haki na haki ilitolewa wakati wa kesi ya awali.

Huku hukumu ya Syed ikibatilishwa, waendesha mashtaka wana siku 30 zijazo kuamua iwapo watawasilisha kesi mpya au waondoe mashtaka dhidi yake.

Waendesha mashtaka wanasema wamewatambua washukiwa wawili “mbadala”, ambao hakuna hata mmoja wao ambaye bado hajatajwa au amewahi kushtakiwa katika kesi hiyo.

Related Articles

Back to top button