Habari

Afande Sele adai wasanii wa Bongo Fleva waliidhalilisha CCM, amtaka Prof. Jay ahame CHADEMA (+audio)

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Afande Sele amefunguka sakata la Chama tawala cha Mapinduzi (CCM) kutangaza wazi wiki iliyopita kuwa hakitawatumia wasanii wa muziki wa Bongo Fleva na Waigizaji wa filamu, Bongo Movies.

Kwa upande mwingine, Afande Sele amemshauri Mbunge wa Mikumi, Professor Jay kuachana na chama chake cha CHADEMA na ajiunge CCM, ili aweze kushinda tena Ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkubwa ujao na kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Afande akimtolea mfano Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe.  Joseph Mbilinyi amesema kuwa ni moja ya wabunge wakorofi ambao wanatamka maneno ya kejeli na matusi kwa Rais Magufuli, kitu ambacho hakileti picha nzuri ndani ya wabunge wa upinzani.

Related Articles

23 Comments

  1. Kuna msanii hata mmoja wa ccm ambae kapata jimbo? Chadema tumewapa wasanii wawili ccm je? Bora uwaambie wasanii waikimbie ccm waje chadema watapata vyeo huko wanachezewa tu kwenye kampen kisha wanaachwa kwenye mataa

  2. Afande sele nikushauri kaka yangu, achana na sugu kumwongelea mama yake, sugu kalelewa na mama yake ni rafiki yake, siyo kama mama yako alikutelekeza na kwenda kuolewa tena, na sugu kakulea wewe kuliko hata mama yako fala wewe

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents