Habari

Afande Sele atangaza kujiunga na CCM, Aeleza sababu

Rapa mkongwe nchini Tanzania, Afande Sele ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi leo Machi 15, 2018 mkoani Morogoro mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Afande Sele

Afande Sele amesema sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kupambana na rushwa na kuwajali wanyonge.

Rais chama chako cha mapinduzi umekisafisha umekivua gamba na ni chama ambacho kimerudi katika uimara wake kama chama cha wanyonge kwa jinsi ambavyo Mhasisi wetu baba wa Taifa alitaka kiwe ndivyo ambavyo umekifanya chamacha mapinduzi leo kimekuwa hivyo Mh. Rais naomba nikupongeze sana kwa hilo lakini kama haitoshi nikuhakikishie kwamba nimeamua kujiunga upande mmoja na wewe ili nisiache na jahazi hili,” amesema Afande Sele, Kwasasa hivi Tanzania kama dereva gari limetulia na linakwenda na mimi kama abiria niache ninywe soda yangu kwa furaha kwa furaha na amani kwasababu naamini chombo chetu kinakwenda salama na sipendi kesho historia ini hukumu niwe miongoni mwa wale ambao hawakuchangia chochote,“amesema Afande Sele.

Hata hivyo, Mfalme huyo wa Rhymes amewaomba wanachama wa Chama cha Mapinduzi wampokee kwa mikono miwili.

Afande Sele kabla ya kujiunga na CCM alishawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA na Chama cha ACT Wazalendo ambapo mwaka 2015 alitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Morogoro Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo.

Rais Magufuli leo Machi 15, 2018 amezindua kiwanda cha kutengeneza sigara cha Philips Moris International mjini Morogoro ambapo Afande Sele alitumia nafasi hiyo kujiunga na CCM.

Related Articles

Back to top button