HabariMichezo

Afisa Habari wa Azam FC afungiwa

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Oktoba 4, 2022 imefungia Afisa Habari na Mawasiliano wa Azam FC, Thabiti Zakaria kwa kipindi cha miezi mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kushutumu waamuzi wa mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons FC uliyopigwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Septemba 30, 2022.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye Kamati hiyo zimedai kuwa Thabiti alitenda kosa hilo huku akifahamu kuwa klabu yake ilikuwa imeshatumia njia sahihi ya kikanuni kwa kuiandikia barua Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kuhusu malalamiko yao kwa Waamuzi.

Kanuni ya 39:(8 & 10) ya Ligi Kuu kuhusu Waamuzi na Kanuni ya 46:(3 & 10) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Viongozi zinasisitiza Klabu kutumia njia sahihi kuwasilisha malalamiko yao kwa TPLB/TFF na kuwataka viongozi kuepuka kulalamika ama kushutumu waamuzi kupitia vyombo vya habari na mahali pengine popote Adhabu hii ni kwa uzingativu wa Kanuni ya 46:10 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Viongozi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents