Afya ya Rais Muhammadu Buhari bado kitendawili

Hali ya Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, inazidi kua kitendawili kwa wananchi wa nchini humo baada ya rais huyo kutoonekana kuweza kuyamudu na kuyatekeleza majukumu yake kama mkuu wa nchi.

Rais Buhari, alikua kwenye matibabu nchini Uingereza mapema mwaka huu, ambapo alikaa kwa takriban wiki sita akiuguza maradhi ambayo bado hayajawekwa wazi na Serikali yake. Hata hivyo, siku ya jana, wanaharakati kutoka katika Asasi za Kiraia wametoa tamko wakimtaka Rais Muhammadu Buhari achukue likizo ya matibabu kutokana na afya yake kutetereka.

Rais Buhari hajahudhuria vikao viwili vya Baraza la Mawaziri hali iliyozua taharuki juu ya afya ya kiongozi huyo.

Mke wa Rais huyo, Aisha Buhari leo amekanusha tetesi za Rais huyo kuugulia maradhi makali kupitia mtandao w twitter na kusema mume wake haumwi kiasi hicho ambacho watu wanahisi. Wananchi wa Nigeria wameanzisha kampeni katika mitandao ya kijamii kwa kiunganishi cha #WhereIsBuhari (Yuko Wapi Rais Buhari).

Related Articles

Back to top button