Habari
Aga Khan afariki Dunia

Bilionea na kiongozi wa kiroho, Prince Karim Aga Khan IV amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88 huko Lisbon, Ureno akiwa amezungukwa na familia yake. Alijulikana kwa kusaidia kujenga shule, hospitali na kutoa umeme kwa mamilioni ya watu katika sehemu maskini zaidi za Afrika na Asia. Aga Khan ambaye ni mzaliwa wa Sweden, aliyekuwa na uraia wa Uingereza, alikuwa Imamu wa 49 wa Waislamu wa Ismailia.