Ahmed Ally atoa la Moyoni kwa Wanasimba
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally ametaka Wanasimba kuwa wavumilivu na kuamini kocha wa kikosi hicho Fadlu Davids.
Ahmed ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa Simba SC imefanya usajili mzuri kuliko mitatu iliyopita hivyo Wanasimba wanatakiwa kuwa watulivu.
“Tumesajili timu bora ndani ya msimu hue lakini ni ngumu kuliona hili kwa sababu mashabiki wa Simba tunatazama mpira kwa presha.
“Presha ya kukosa Mataji misimu mitatu inatunyima uhuru wa kuangalia mpira kwa jicho la utulivu ndio maana ligi haijaanza lakini tumeanza kuona baadhi ya wachezaji hawafai kwa sasa Wanasimba tunahitaji ushindi tu na tunahitaji kila itu afunge hit yote ni presha ya mataji’. AMEANDIKA Ahmed.
Ahmed aliendelea kuandika kuwa “Ombi langu kwenu wana Familia ya Simba tuwe na subira na wavumilivu tumpe uhuru Mwalimu na tuwape nafasi wachezaji wetu kuonesha uwezo wao”, aliongeza