Mitindo

Aina ya mavazi yaliyo bamba kwa mwaka 2017

Hello nakukaribisha katika habari za mitindo hapa Bongo5, kama ilivyoada kwetu kuhakikisha tunakupa habari zenye uhakika. Ikiwa tunaenda kuumaliza mwaka 2017 Bongo5 inakuletea orodha ya nguo zilizovaliwa katika kipindi cha mwaka huu.


Aina ya nguo hizo ni :-

Track suit:

Idadi kuwa ya watu hasa vijana kwa mwaka huu wamevaa sana track suit na wengi wameonyesha kufurahia vazi hili. Wapo ambao walivaa full na wapo ambao walivyaa suruali na top nyingine.

Kama ni mfuatiliaji mzuri sana wa mitindo na hasa upande wa burudsani utagundua kati ya wasanii kumi lazima nane kati yao wametinga vazi hili. Mtu kama Jackili wolper alitinga, Diamond Platnumz, Bill Nas, Harmonize, Rayvanny, Jokate, Feza Kessy na wengineo.

Nguo za vitenge (Magauni, blauzi, tops na suruali)

Kama mpaka leo huana nguo ya kitenge duuh!! tukupe pole lakini pia uhakikishe unajiapatia yako. Kwa sasa vazi la kitenge linazidi kukamata soko toka lilivyorudi sokoni miaka miwli iliyopita na limekuwa likitumika kwa watu wa rika zote.

Huwenda mwakani tukija na ushonaji mpya wa vai hili basi litazidi kukaa sokoni muda mrefu.

Magauni ya kuburuzika:

Magauni haya ya kuburuzika na kubana yaliongozwa kuvaa na msataa wa filamu na video vixer katika event mbali mbali. Mfano Wema alivyaa gauni hili katika photoshoot na pia katika uzinduzi wa filamu yake ya ‘Heven Sent’ ambapo aliigiza na Gabo.

Wengine ni Sanchoka, Lulu, Jokate, Hamisa Mobeto, Zari the Boss Lady, Esma Platnumz na wengineo.

Flower Jeans na Ripped Jeans:

Flower Jeans na Ripped zimeongoza kuvali sana kwa mwaka huu kwani hadi wa kaka nao walitinga Flower Jeans mwaka huu. Kama utak,mbuka video ya Pantoranking ft Diamond ya ‘Love You Die’ alitinga Flower Jeans.

Pia ukizunguka katika video tano hizi huwexzi kukosa msanii aliyevaa Ripped Jeans ama jinsi ya kuchanwa chanwa ambayo ipo kwenye soko kwa zaidi ya miaka mitatu na inafanya vizuri huwenda mwakani ikaendelea kuwepo.

Pensi (Kaptula):

Moja ya msani aliyeongoza kuvaa kaptula ama vipenzi mwaka huu ni Alikiba mzee wa ‘Seduce Me’. Mkali huyu wa Bongo Flava ametikisha kwa kutinga vipensi tofauti tofauti na vilikuwa vikimtoa.

Vijana wengi huwenda walikuwa na hofu ya kuvaa kaptula ila Ali aliwapao ushawishi na mpaka sasa wanajiachia navyo kitaani.

Off Shouder (Blauz na magauni):

Yeees! wale wenye mabega na mikono mizuri walifaidi nguOo hii mwaka huu, ambayo iliwanyima nafasi vibonge kuonyesha mabega yao.

Ni nguo nzuri kwa mtu ambaye ana mwili wa wastaa kwani ilikuwa haitaki mtu aliye na mwili mkubwa na wenye michirizi avae nguo hii kwani asinge pendeza.

Jamsuit:

Kwa wisio na vitambi vikubwa na na vya watani walivyaa Jumsuit za tofauti tofauti kama za jeans na vitambaa. Ilivali wa japo sio kwa silimia kubwa sana ila natumai mwakani itabamba kinoma noma.

Unaweza kuongeza list ya vazi unaloamini limevalika sana mwaka huu na unalitabiria makubwa mwaka 2018.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents