Fahamu

Air Tanzania kuanza safari zake kuelekea Guangzhou China tarehe hii

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Linatarajia kuanza kufanya safari zake kuelekea jijini Guangzhou China ifikapo tarehe 20 Machi.

Hatua hiyo inakuja wakati kukiwa na vizuizi vya kusafiri vilivyowekwa duniani kutokana na janga la virusi vya corona.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi aliliambia gazeti la Citizen Ijumaa kuwa safari za ndege kwenda china ambazo ziliahirishwa tangu mwezi Septemba mwaka jana kwa sababu ya janga la corona zitaanza rasmi mwezi huu.

”Tutasafiri kwa wiki mara moja Jumamosi saa 11 asubuhi kuelekea China na kurejea Tanzania siku ya Jumapili saa 11,” alisema.

Shirika hili limeandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii taarifa kuhusu safari hizo zinazotarajiwa kuanza

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents