Habari

Ajali ya ndege yaua watu 10 Sudani Kusini

Mamlaka za Sudan Kusini zimethibitisha kuwa ndege ndogo imeanguka siku ya Jumanne jioni katika jimbo la mashariki la Jonglei , na kusababisha vifo vya watu 10 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Ilitokea katika uwanja wa ndege wa Pieri muda mfupi baada ya kuruka ilipokuwa ikielekea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba.

Timu ya wachunguzi ilipelekwa kwenye eneo la tukio kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa awali, Waziri wa usafirishaji Madut Biar Yel alisema.

Ndege hiyo inamilikiwa na kampuni ya binafsi , South Supreme Airlines.Kampuni hiyo haijazungumza chochote kuhusu ajali hiyo.

Gavana wa jimbo la Jonglei Denay Jock Chagor amesema alipokea taarifa kwa ”mshtuko na uoga” na kutuma salamu za rambirambi kwa familia na marafiki wa marehemu.

Kwa mujibu wa BBC. Usalama wa anga la Sudani Kusini bado haujakadiriwa na Mpango wa Kimataifa wa Tathmini ya Usalama wa Anga.

Lakini data kuhusu mtandao wa usalama wa anga,(ASN) inaonesha kuwa takribani ndege 10 zilianguka katika maeneo tofauti nchini Sudani Kusini kati ya mwaka 2018 na 2020, na kusababisha vifo karibu 30.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents