Habari
Ajali ya Ndege yazua kizaazaa

Ndege iliyokuwa imebeba watu 80 ilianguka jana wakati wa kutua katika uwanja wa ndege wa Toronto Pearson, Canada na kusababisha angalau watu 18 kujeruhiwa.
Video kutoka eneo la tukio ilionyesha ndege ya Delta Air Lines ikiwa imegeuka juu chini kwenye barabara ya kurukia iliyofunikwa na theluji, huku watu wakiondoka kutoka eneo hilo. Imaelezwa kuwa watu wawili waliokuwa katika hali mahututi walihamishwa kwa helikopta hadi kituo cha matibabu ya majeraha.

Ndege namba 4819 – inayoendeshwa na Endeavor Air, kampuni tanzu ya Delta – ilianguka wakati wa kutua Toronto ikisafiri kutoka Minneapolis, jimbo la Minnesota, Marekani.