
“Ni heri kuwahi kuliko kuchelewa.” Kwenye ulimwengu wa ajira kauli mbiu hii imekuwa ya wengi sana haswa Katika dunia ambayo waajiri hulalamikia uchelewaji vilevile mara nyingi kuwahi katika usaili huonekana kama ishara ya nidhamu na kujituma kwa waomba ajira ili kujiongezea nafasi ya kuajiliwa, lakini hii imekuwa tofauti kwa kijana mmoja huko Marekani ambapo kuwahi kwake kwa dakika 25 kabla ya muda rasmi wa usaili kuligeuka kuwa tiketi ya yeye kukosa kazi.
Kupitia mtandao wa Linkedin Mmiliki wa kampuni ya usafi mjini Atlanta, Matthew Prewett aliweka wazi kuwa alikataa kumuajiri kijana huyo kwa sababu alifika mapema mno kwenye usaili wa nafasi ya msaidizi wa ofisi ambapo alidai kuwa kijana huyo alifika dakika 25 kabla ya muda na kufanya hiyo kuwa moja ya sababu kubwa za kutomchagua.
Alifafanua kuwa ingawa kuwahi ni jambo jema lakini kufika mapema kupita kiasi kunaweza kuashiria kutokuwa na uelewa wa kijamii au kudhani unapaswa kupewa kipaumbele vilevile alisema uwepo wa kijana huyo mapema ulimlazimisha aharakishe kazi zake na kumfanya ajisikie kukosa faragha Ofisini kwake.
Chapisho hilo lillibua mjadala mkali mtandaoni ambapo baadhi ya Watu walimuunga mkono Mwajiri huyo lakini wengi walimtetea kijana huyo wakisema labda alikuwa anaogopa kuchelewa au hakuwa na usafiri wa uhakika hivyo kuwahi kwake inapaswa kuonekana kama juhudi na si kosa aliandika mtumiaji mmoja.
Wengine walienda mbali zaidi na kusema wangempatia kazi mara moja kwa kuonyesha namna alivyothamini muda lakini kwa Prewett ambaye ndie muajiri ujumbe ulikuwa wazi akisisitiza kwamba kuwahi ni vizuri lakini kuwahi mno kunaweza kugharimu zaidi ya unavyodhani.