Burudani
Barakah The Prince aeleza kuhusu ujio wa albamu yake mpya
Msanii wa muziki kutoka RockStar4000, Barakah The Prince amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya ujio wa albamu yake ya kwanza.
Muimbaji huyo amesema albamu hiyo huwenda ikatoka katikati ya mwaka huu au mwisho wa mwaka kutegemea na maandalizi na uwamuzi wa label yake.
“Albamu yangu ya kwanza inatoka chini ya RockStar4000 na itatoka mwaka huu katikati au mwishoni,” Barakah The Prince alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV.
Alisema kila msanii wa label hiyo ana mipango yake na hawafanyi vitu kwa kuigana kwa sababu fulani kafanya.
Muimbaji huyo alisema hata wakati wake wa tour za kimataifa ukifika anaonekana akisafiri kama wasanii wengine wa label hiyo.