Albania: Wabunge wamkataa Rais Ilir Meta

Wabunge nchini Albania wamepiga kura ya kumtimua rais Ilir Meta, wakimtuhumu kwa kuvunja sheria za ofisi yake kwa kuungana na upinzani wakati wa kampeni ya uchaguzi mwezi Aprili.

Ofisi ya rais Meta ilipuuzilia mbali mara moja kura hiyo ya wabunge ikisema ni uamuzi unaokwenda kinyume cha sheria na wa kijinga.

Mahakama ya Katiba ina miezi mitatu kuridhia au kuukataa uamuzi huo, lakini kabla ya hapo Meta ataendelea kushikilia wadhifa huo.

Meta na Waziri Mkuu Edi Rama walikabiliana mara kwa mara wakati wa kampeni kali ya uchaguzi. Alimtuhumu Meta kwa kuwa kiongozi wa kimabavu na fisadi, mashambulizi ambayo yalipingwa na waziri mkuu huyo.

Pia aliahidi kujiondoa katika wadhifa wa rais ambao hauna madaraka makubwa kama wasoshalisti wangeshinda uchaguzi, na wakashinda. Baada ya uchaguzi, tume ya bunge ikaundwa kuchunguza tabia ya rais.

Related Articles

Back to top button