Muziki

Album ya Alikiba yafikisha wasikilizaji zaidi ya mil 17 katika hii mitandao mitatu

Kila mmoja anafahamu kuwa staa wa Bongo Fleva na CEO wa lebo ya Kings Music Alikiba aliachia album yake tarehe 7/9 mwaka huu inayojulikana kwa jina la THE ONLY ONE KING yenye ngoma 16.

Katika ngoma hizo 16 aliachia na video moja ya Oya Oya, album hiyo inaonekana kupokelewa kwa kasi sana na mashabiki wa muziki dunaini kote kwani takwimu zinazidi kuwa kubwa baada ya kuachiwa tu.

Zifuatazo ni takwimu za mitandao (Platform) mitatu ya kuuzaia nyimbo ambayo ni Audimack, Spotify na Boomplay.

Katika mtandao wa Boomplay tayari album hiyo imefikisha zaidi ya Streaming mil 10.

Katika mtandao wa Audimack album hiyo imefikisha Streaming mil 7.

Katika mtandao wa Spotify ina straming zaidi ya mil 1.5 mpaka hivi sasa.

Huku ikifikisha Streaming zaidi ya mil 18 katika mitandao hiyo mitatu.

Related Articles

Back to top button