Album ya Marioo The Godson imebakiza siku 14 tu (Video)

Omary Mwanga alimaarufu @marioo_tz kwa sasa sio jina lenye uwalakini tena kwenye game ya muziki wa Bongo Fleva hasa Afrika Mashariki.
Ni msanii ambaye tayari amejenga Uaminifu kwa Watanzania na wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva kwa sasa na mashabiki zake.
Inawezekana ukitaja wasanii watatu Bora kwa sasa kwa hiki kizazi jina la @marioo_tz lazima lije la kwanza.
Sio hivyo tu wiki kadhaa nyuma ametoka kujishindia Tuzo ya msanii bora wa Bongo Fleva na Muandishi bora wa Bongo Fleva kupitia Tuzo za TMA akiwashinda wasani wakubwa tu hapa nchini.
Hapo ameshinda Tuzo hizo bila Album ni kupitia nyimbo alizotoa nje ya album iliyopita na sasa anakuja na album ya The Godson, anaweza kuondoka na Tuzo myingi sana mwakani.
Kwa sasa @marioo_tz akitangaza anaachia ngoma lazima watu washtuke na watege masikio yao kuona @marioo_tz anakuja na kitu gani?? Maana anakubalika sana kwa sasa.
The GodSon itakuwa album yake ya pili kwenye maisha yake ya Kimuziki kwani mwaka 2022 aliachia album ya THE KID YOU KNOW ambayo ilikuwa miongoni mwa album bora na ni miongoni mwa album zilizotengeneza numbers nyingi sana kwenye platforms za Muziki.
Album hiyo ilitoa hits nyingi sana kama kama I miss You akiwa na Alikiba, Anisamehe akiwa na Rayvanny, Siwezi, Dear Ex, Mi Amore, My Life, Sina baya na zingine.
Watu wengi wanatamani kumuona @marioo_tz kwenye level zingine kwa maana level za Muziki wa Ushindani Kimataifa na huenda THE GOD SON ikawa ndio shuluhisho la Yote haya.
Mpaka sasa wengi wanaisubiria kuipna na kuisikia album ijayo ya Marioo ambayo inatoka November 28 ambapo zimebaki siku 14 tu kufika siku hiyo.
@marioo_tz amebeba matumaini ya Watanzania wengi na wanatamani kumuona kwenye level za Akina Rema, Asake na wengine maana ana uwezo huo.
Wengi wanatamani kuona collabo zake zipoje?? Amefanya na wasanii gani?? Je wasanii hao wa Nje tu au wa ndani tu au mchanganyiko??
Msanii gani unahisi hawezi kukosekana kwenye album ya @marioo_tz ijayo???
Imeandikwa na @el_mando_tz