Habari

Algeria, Nigeria na Niger zakubaliana kuuza gesi Ulaya

Mawaziri wa nishati wa Algeria,Nigeria na Niger wametia saini makubaliano juu ya ujenzi wa bomba la gesi kupitia kwenye jangwa la Sahara ili kupeleka gesi barani Ulaya.

Baada ya ujenzi kukamilishwa bomba hilo la kilometa 4000 litakuwa na uwezo wa kuleta kubiki mita bilioni 30 barani Ulaya kwa mwaka. Bomba hilo litakalojengwa kwa gharama za dola bilioni 13 litaanzia Nigeria na kupitia Niger hadi Algeria.

Na kutokea hapo gesi itapitishwa kwenye bomba la chini ya bahari ya Mediterrania hadi Ulaya au itapakiwa kwenye matanki ya gesi ya kioevu na kusafirishwa hadi barani Ulaya.

Nchi za Umoja wa Ulaya zinakusudia kuondokana na kuitegemea Urusi kwa ajili ya mahitaji ya nishati. Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema lengo la mradi huo ni kuepuka nchi za jumuiya hiyo kushinikizwa na Urusi.

Related Articles

Back to top button