Habari

Alichozungumza Rais Samia na Papa Francis

Rais Samia Suluhu Hassan jana alikutana na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Papa Francis mjini Vatican na kuzungumza mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya elimu, afya, ustawi wa jamii pamoja na changamoto ambazo Tanzania inapitia kwa sasa.

Aidha wawili hao pia walijielekeza zaidi katika masuala ya kijamii, kikanda, kimataifa pamoja na umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa katika kujikita kudumisha amani ulimwenguni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Holy See Press Office mazungumzo ya viongozi hayo ambayo yalikuwa ya faragha yaliyodumu kwa takribani dakika ishirini na tano (25) wameridhika na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican Na Tanzania; Mchango wa kanisa katoliki katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu hususan katika sekta ya elimu, afya na ustawi wa jamii pamoja na changamoto ambazo Tanzania inapitia kwa sasa.

Takwimu zinaonesha kwamba, kanisa Katoliki nchini Tanzania linamiliki na kuendesha shule za awali 240, shule za msingi 147, shule za sekondari 244, vyuo vya ufundi, vyuo vikuu 5; taasisi za elimu ya juu 5 na vituo vya vyuo vikuu 2 ambavyo viko chini ya chuo kikuu cha mtakatifu Agustino, SAUT.,ambapo vyuo vyote hivi vina jumla ya wanafunzi 31, 000 pamoja na taasisi za afya 473.

Imepita takribani miaka 12 tangu rais mstaafu jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea mjini Vatican na kukutana na baba mtakatifu Benedikto Xvi tarehe 19 Januari 2012.

Katika mazungumzo ya dakika kumi na tano, viongozi hawa wawili waligusia kuhusu: Majadiliano ya kidini, amani katika eneo la Maziwa Makuu, Afya, Ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Ni katika muktadha wa kujenga na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Vatican, tarehe 12 Februari 2024, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican.

Baadaye, Rais Samia amebahatika pia kukutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents