Burudani

Alicios aeleza ujio wa ngoma yake mpya pamoja na albamu mwaka huu

Baada ya kufanya vizuri kwenye ngoma mpya aliyoshirikishwa na Bushoke, msanii Alicios Theluji ajipanga kuachia wimbo wake mpya Julai mwaka huu pamoja na ujio wa albamu yake.

Akiongea na Bongo5 Jumatano hii, msanii huyo amesema ataachia ngoma yake mpya mwezi huo akiwa pamoja na video yake ambapo kila kitu kimefanyika hapa hapa nchini Tanzania.

Alicios ameongeza kuwa mwishoni mwa mwaka huu anatarajia kuachia albamu yake mpya ambayo itakuwa na ngoma chache ambazo amewashirikisha kutoka Afrika kolabo chache na wasanii kutoka Afrika tutegemee ujio wa wimbo wake Mpya wakati wowote.

Wakati huo huo msanii huyo anatarajia kuanza kufanya ziara yake ya kimuziki katika bara la Ulaya ikiwa ni mara yake ya pili kufanya hivyo tangu aanze muziki.

Related Articles

Back to top button