Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariMichezo

Alikiba amshukuru Harmonize, kwa kuwasapoti SAMAKIBA

Alikiba amshukuru @harmonize_tz na kueleza sababu ya kukosekana kwake. Baada ya mchezo wa leo kati ya Timu Kiba na Timu Samatta @officialalikiba amemshukuru @harmonize_tz kwa kutamani kucheza mchezo siku ya jumamosi.

Ikumbukwe kuwa Harmonize aliomba kushiriki mchezo huo wa SAMAKIBA na aliamua kuchezea timu Samatta kabla ya ratiba zake kuingiliana.

Harmonize aliahidi kuwa Alikiba hatopita kwenda kufunga endapo angepangwa yeye kuchezea timu Samatta.

Baada ya Alikiba kusikia hayo kwenye press ya mwisho kuelekea mchezo huo Alikiba alimuomba Samatta ampangea Harmonize ili akapambane naye uwanjani inagwa Samatta alisema ratiba zimeingiliana alikuwa na Show Congo.

Baada ya mchezo kumalizika ambapo timu Kiba waliimbuka na ushindwi kwenye matuta ya penati ambapo ndani ya dakika 90 mchezo ulimalizika kwa matokeo ya sare ya goli 3-3.

Alikiba alimshukuru Harmonize kwa kuamua kujitolea kwenye mchezo huo.

Related Articles

Back to top button