Alikiba wa moto 2021, back to back ngoma tatu ndani ya wiki tatu (+ Video)

Msanii wa muziki wa bongo Fleva Alikiba ameuanza vizuri mwaka 2021 kwa kufanya kazi nyingi mpaka hivi sasa tangu mwaka huu uingie.

Alikiba tayari ameonekana kwenye ngoma tatu tofauti ndani ya wiki tatu, ikumbukwe aliahidi kuwa sas ahivi ni mwendo wa back to back mpaka mashabiki wake wachoke.

Alikiba ameanza hivyo baada ya kushirikishwa ndani ya ngoma tatu mfululizo lakini pia akiahidi kuwa mwaka huu ataachia album yake katikati ya mwaka huu.

Alikiba ngoma yake binafsi ya mwisho ilikuwa ni MEDIOCRE ambayo aliiachi mwezi wa tisa lakini baada ya hapo sasa hivi amejitokeza katika ngoma tatu tofauti za kushirikishwa, alianza na ngoma ya DJ Sbu kutoka Afrika kusini katika ngoma  ya NAKUEPNDA wiki mbili zilizopita na baada ya wiki moja tena alijitokeza kwenye ngoma ya PROUD OF YOU aliyoshirikishwa na Darassa lakini siku moja iliyopita ameshirikishwa na msanii kutoka kenya Otile Brown katika ngoma ya Inlove.

Tuambie ngoma ipo ambayo Alikiba ameshirikishwa umeipenda kuliko zote.

Dondosha comment yako hapo chini na weka Emoji za moto kwa Alikiba kwa kuanza mwaka vizuri.

 

Related Articles

Back to top button
Close