Burudani
Alikiba awaonyesha mashabiki wake picha za video yake mpya (Picha)

Alikiba anatarajia kuwapa mashabiki wake zawadi waliyoisubiri kwa muda mrefu – video.
Muimbaji huyo ameshoot video nchini Afrika Kusini na muongozaji Meji Alabi.
Kupitia ukurasa wa Facebook, Alikiba amepost na utengenezaji wa video hiyo na kuandika: Music video shoot in South Africa at 3 degrees celsius… We keep rolling!
Muongozaji Meji Alabi akiwa kazini
Hivi karibuni mashabiki wa Alikiba walilalamika kuchelewa kwenye video ya Chekecha na kudai kuwa anawaangusha.