BurudaniHabari

Alikiba kimataifa ameshakata tamaa pia ameridhika – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake pendwa cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ametoa maoni yake kuhusu muziki wa staa wa muziki wa Bongo Fleva Alikiba kuhusu kama anafanya muziki wa ushindani Kimataifa au laah.

@el_mando_tz akijibu baadhi ya comment za mashabiki waliouliza kama Alikiba anafanya muziki wa ushindani Kimataifa kama tulivyoona baadhi ya wasanii wakifanya nyimbo zao na kwenda kimataifa pia kusikilizwa na kuingia kwenye baadhi ya chat za muziki nje ya Afrika kama Diamond kupitia wimbo wake wa SHU na pia Harmonize kupitia Single Again.

@el_mando_tz anasema kuwa kwa namna Alikiba anavyoonekana na namna muziki wake unavyofanya kupitia platform mbalimbali inaonyesha yeye mwenye hata tena muziki wa Kimataifa bali ameamua kuwapa tu muziki mzuri mashabiki wa Tanzani na Afrika Mashariki.

Anatolea mfano nyimbo kama Aje, Seduce Me na Mwana Dar Es Salaam ambazo zilifanya vizuri na kumpatia tuzo ya MTV EMA mbele ya Wizkid, Diamond na Davido ndio ambazo zilifika mbali zaidi.

Lakini nyimbo zake za sasa ni ngumu kuona zikishindana na nyimbo za wasanii wakubwa Afrika na duniani tofauti na zamani, lakinni pia Alikiba ana muda sasa hajafanya show za kimataifa kama zamani na show zake za mwisho ilikuwa Marekani miaka miwili iliyopita baada ya kuachia album ya Only One King na baada ya hapo hakuna tena zaidi ya kwenda Kenya.

Mbali na hayo pia hatujamuona Alikiba kwenye tuzo nyingi kubwa za Afrika ambazo alikuwa anaingia zamani, kwa mfululizo wa matukio hayo inakupa picha kuwa Kimataifa kama kumeanza kumsusa Alikiba.

Unakubaliana na @el_mando_tz ??

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents