Burudani
Alikiba ataja vitu anavyohitaji apewe akiwa kwenye tour

Wasanii wakubwa wanapoenda sehemu kwaajili ya show huwa na mahitaji yao muhimu wanayomtaka promota ayazingatie. Wapo wenye mahitaji mengi na magumu lakini kama unamtaka huna budi kuyatimiza.
Tumemuuliza Alikiba kwenye mahojiano tuliyofanya naye kutaka kujua yeye anahitaji nini anapoenda kwenye tour. Na hivi ndivyo alivyosema.
1.Gari nzuri ya mwaka ambao upo latest, gari yenye hadhi, siwezi kuzitaja lakini wakati nataka kuchagua kwenye mkataba ndio huwa nazitaja. Napenda gari jeusi
2. Hoteli ni five stars
3. Ndege napanda business class
4. Ulinzi, pawe safe kutokana na mazingira yalivyo
5. Chakula kizuri