Alikiba,Bien kumfunika Sea Poul kuimba live? Wasanii hawajui kufanya show
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameizungumzia Show kubwa itakayofanyika Wikiendi hii ambayo imekusanya wasanii wakubwa kama mkongwe Sean Paul kutoka Jamaica, Alikiba, Jaivah, Nandy Tanzani, Bien Kenya na wengine.
Anasema ujio wa Sean Paul utakuwa na faida kubwa sana kwenye upande wa Kiwanda cha Muziki cha Bongo Fleva kwa ujumla.
Mbali na hilo wasanii watakaotumbuiza lazima wafanye jambo na Sean Paul asiondoke hivi hivi lazima akautangaze muziki wetu Nje kama wataweza hata collabo itokee.
Anaongeza kuwa Show hiyo tunategemea kuona ubora tu kwenye Pafomansi za wasanii hasa kuimba Live Jukwaani.
Kwa upande wa Alikiba na Bien hilo halina shaka maana ni wazoefu wa muda mrefu sana tena inawezekana wao wakafanya Show kali kuliko Sean Paul maana Wasanii wengi wa Ulaya na America hawapendelei kuimba Live.
Lazima wasanii waonyeshe ubora maana show hiyo itakuwa inamulikwa duniani kote kupitia ujio wa Sean Paul.
Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman & Editor @samirkakaa